Ad imageAd image

Jubilee Holding Limited, Kampuni inayotoa huduma za Bima kupitia Kampuni zake tatu (Jubilee Life Insurance, Jubilee Health na Jubilee General – Allianz) zapongezwa kwa kuongeza watumiaji Bima za Maisha.

Highlights
  • "Bima kama soko liko salama, makampuni yanasimamia vizuri na wawekezaji wanaongezeka, makampuni yanajisajili kufanya biashara ya bima yameongezeka kwa asilimia 11 mwaka huu, kwahiyo mwamko wa watu kutumia bidhaa za bima umeongezeka hususani bima za maisha" Amesema Dkt. Saqware.

Kampuni ya Jubilee Holding Limited imekuwa ikifanya kazi katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka 85 hadi sasa, huku dhumuni kuu likiwa kulinda maslahi ya biashara, watu binafsi, taasisi na kampuni kwa kutoa huduma bora zinazolenga kukidhi mahitaji yao ya bima ikiwa ni pamoja na bima za Maisha, Afya, Moto, Magari na kadhalika.

Hayo yameelezwa leo Januari 5, 2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima za Maisha ya Jubilee Bi. Helena Mzena katika hafla ya kuwatunuku zawadi ya milioni sita na elfu sabini na tano (kwa kila mmoja) washindi watano ambao ni wanafunzi walioshiriki katika shindano la uchoraji wa shule za serikali lililofanyika mwaka 2017 wakati taasisi hio ikiadhimisha miaka 80 ya utoaji huduma nchini. Washindi hao ni Salma Musa, Atupele Westoni Ezrael, Petro Joseph Mwakyeme, Ibrahim Miraj Zingira and Khadija Mohamed.

“Dhumuni kuu ni kulinda maslahi ya biashara, watu binafsi, taasisi na kampuni kwa kutoa huduma bora zinazolenga kukidhi mahitaji yao ya bima ikiwa Bima za maisha, moto, magari” Amesema Bi. Helena

Aidha ameongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora za bima ili kuhakikisha Watanzania wote wanafurahia huduma hizo.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa hafla hiyo Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware amesema watanzania wanapaswa kutumia bima ya maisha ya elimu katika kuwasaidia wanafunzi kufanikisha malengo yao ya kielemu.

“Tunatoa rai kwa watanzania wote, wazazi wenye watoto ambao wameanza shule wanaotarajia kuanza shule kukata bima ya maisha ya elimu, bima hizi zinapoiva zitumike kama kulipia gharama za elimu, ikiwemo ada, mavazi na gharama zingine zote za shule ili mtoto wako asome shule nzuri,karibu utumie bima za maisha” Amesema Dkt. Saqware.

Katika hatua nyingine ameeleza hali ilivyo ya mwamko wa watanzania katika kukata bima za maisha.

“Bima kama soko liko salama, makampuni yanasimamia vizuri na wawekezaji wanaongezeka, makampuni yanajisajili kufanya biashara ya bima yameongezeka kwa asilimia 11 mwaka huu, kwahiyo mwamko wa watu kutumia bidhaa za bima umeongezeka hususani bima za maisha” Amesema Dkt. Saqware.

“Makampuni yamefanya vizuri sana hasa kampuni ya Jubilee, na kampuni zingine za maisha zinaendelea kuongeza wateja na watumiaji wa huduma za bima za maisha,”

“Nitoe rai yangu kwa watanzania watumie bima za maisha kwa sababu ni uwekezaji na urithi mkubwa sana kwa watoto, na kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja” amesisitiza Dkt. Saqware.

Kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma kupitia Jubilee General Allianz, Jubilee Life Insurance Corporation na Jubilee Health Insurance.

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner