Ad imageAd image

Gavana Tutuba apokelewa na Gavana mstafu wa zamani wa BoT

Highlights
  • Gavana Emmanuel Mpawe Tutuba anakuwa Gavana wa Nane wa Benki Kuu ya Tanzania yangu nchi yetu ipate Uhuru 1961.

Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. EMMANUEL MPAWE TUTUBA, amelakiwa na Gavana Mstaafu, Prof. FLORENS LUOGA alipowasili kwa mara ya kwanza Makao Makuu ya BoT jijiji Dodoma ikiwa ni saa chache baada ya Kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma IKULU, Chamwino.Wengine waliomlaki Gavana Tutuba ni Manaibu Gavana pamoja na wafanyakazi wa BoT.

Gavana Emmanuel Mpawe Tutuba anakuwa Gavana wa Nane wa Benki Kuu ya Tanzania yangu nchi yetu ipate Uhuru 1961.

Gavana wa kwanza alikuwa Bw. Edwin Mtei aliyeongoza Benki Kuu kuanzia Juni 1966 hadi Januari 1974.

Alifuatiwa na Bw. Charles Nyirabu aliyehudumu kuanzia Januari 1974 hadi Januari 1989. Gavana aliyefuatia ni Bw. Gilman Rutihinda kuanzia Januari 1989 hadi Januari 1993.

Gavana Rutihinda alirithiwa na Dkt. Idris Rashid kuanzia Januari 1993 hadi Januari 1998. Kuanzia Januari 1998 Benki Kuu ya Tanzania iliongozwa na Dkt. Daudi Ballali hadi Januari 2008 na kufuatia na Profesa Benno Ndulu aliyeongoza kuanzia Januari 2008 hadi Januari 2018.

Kuanzia mwaka 2018 Benki Kuu ya Tanzania iliongozwa na Profesa Florens Luoga ambaye amehudumu hadi Januari 2023.

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner