Ad imageAd image

Matumaini mapya kwa wadau wa habari muswada wa marekebisho ya sheria ya habari kusomwa bungeni Leo

Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 utasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni leo Ijumaa Feubuari 10 kutokana na kuondolewa kwa Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote unaoendelea na majadiliano.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amethibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma  kutokana na awali kuelezwa usingesomwa huku akisisitiza kuendelea kuaminiana baina ya Serikali na Vyombo vya Habari nchini.

Waziri Nape amebainisha kuwa katika mchakato wa marekebisho  ya sheria hiyo wadau wa habari wamepata fursa ya kuwasilisha maeneo ambayo wanataka yarekebishwe ambao wamekutana na viongozi wa serikali na kufanya majadiliano.

” Nliongoza kikao cha pamoja kati ya wizara na wadau wa habari kilichofanyika Novemba 21, 2022 ambapo yaliwekwa makubaliano ya pamoja upande wa serikali na upande wa wadau juu ya mapendekezo ya maeneo yatakayofanyiwa mapendekezo ” 

Febuari 07, 2023 Msemaji wa serikali Gerson Msigwa alitoa taarifa kwamba muswada huo utawasilishwa bunge lijalo  kutokana na muda kuwa mdogo hautaweza kuwasilishwa mpaka bunge lijalo ambalo linatarajiwa kuwa mwezi wa nne.

Kufuatia taarifa hiyo ya msemaji wa Serikali Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF lilitoa tamko la kupokea kwa masikitiko taarifa hiyo ya kushindikana kuingizwa bungeni kwa muswada wa marekebisho ya sheria ya huduma za habari.

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner