Ad imageAd image

NBC na Jubilee Allianz kutoa elimu ya Bima kwa Mawakala

Mkuu wa kitengo cha Bima Kutoka NBC, Benjamin Nkaka amesema NBC kwa kushirikiana na Jubilee Allianz itaendelea kutoa elimu ya BIMA kwa mawakala nchini ili kuongeza urahisi wa upatikanaji na kukuza soko la Bima nchi nzima huku akisema wanatarajia hadi kufikia mwezi wa sita kutoa mafunzo kwa mawakala wasiopungua 6000.

Ameyabainisha hayo  wakati akikabidhi vyeti kwa mawakala wa Benki ya Biashara NBC zaidi ya 100 waliofanya mtihani na kufaulu ikiwa ni wiki chache zilizopita baada ya kupatiwa mafunzo ya uuzaji Bima Kukamilika.

“Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz kushirikiana na Benki ya NBC, ilichagua mawakala wa huduma za kifedha, kuwadhamini na Kuwapeleka mafunzo ya muda mfupi katika chuo cha Africa College of Insurance and Social Protection kwaajili ya kupatiwa elimu ya Bima.” amesema Nkaka.

Aidha Nkaka amesema matarajio yao kwa wahitimu ni kutoa huduma bora kwa wateja, kuwapa elimu na kuhakikisha kuwa wanasogeza Zaidi huduma ya BIMA kwa wateja wao.

Kwa upande wake Meneja Mkuu msaidizi wa Jubilee Allianz, Abullatif Suleiman, amesema kwa sasa ukuaji wa bima katika soko ni mdogo na kupelekea kampuni ya Jubilee Allianz pamoja na Benki ya Biashara NBC kuingiza mawakala katika huduma hiyo ya kuuza Bima.

“Sisi kama Jubilee Allianz tunaona ni fursa kubwa, nyinyi mnapokea wageni wengi katika vituo vyenu na katika hili hatutowaacha pekeenu, sisi na NBC tutakuwa tunawapitia katika vituo vyenu kuhakikisha mnaweza kuuza na kutatua changamoto mnazokutana nazo.”amesema Nkaka.

Naye Mkurugenzi wa mafunzo na taaluma kutoka ACISP, Ansium Anseum amesema wataendelea kutoa mafunzo na kuwawezesha mawakala hao ili waweze  kutoa huduma bora za bima nchini kote.

Meneja wa mawakala wa Bima kutoka NBC, Janeth Sindano amesema kwa sasa NBC ina  zaidi ya mawakala 9500 ambao wanapatikana nchi nzima na kusema kuwa watakuendelea kushirikiana katika uuzaji wa bima kupitia jubilee allianz.

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner