Ad imageAd image

Kioo kuwa miongoni mwa Bidhaa zitakazotangulia AFCFTA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.)amekishauri Kiwanda cha Kioo Limited kuendelea kuzalisha bidhaa za kioo kwa wingi na zenye ubora na viwango vinavyohitajika kwa ajili ya Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Aidha, amekishauri Kiwanda hicho kuzalisha bidhaa za kioo zitakazotumika kama vifungashio kwa ajili ya wajasiliamali wadogo wadogo ili waweze kuhimili ushindani katika biashara na kuweza kuingia katika soko la AfCFTA.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha Kioo Limied kilichopo Chang’ombe, jijini Dar es Salaam 14/02/2025 kwa lengo ya kuangalia bidhaa za kioo zinazozalishwa na kiwanda hicho zinazotarajiwa kuingizwa katika soko la AfCFTA.

Aidha, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi nane za mwanzo zilizopewa kipaumbele cha kupeleka bidhaa kwenye soko hilo ambapo miongoni mwa bidhaa 10 zitakazotangulia kuingia katika soko hilo kuanzia Julai Mosi 2023 ni pamoja na Kahawa, Marumaru na Kioo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bwana Kumar Krishnan amesema Kiwanda cha Kioo kiko tayali kuingiza bidhaa ya kioo katika soko la AfCFTA kwa kuwa kiwanda hicho kinauwezo wa kizalisha zaidi ya chupa milioni moja (1) kwa siku ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.

Aidha ameeleza kuwa kiwanda hicho kinatengeneza kioo kwa kitumia malighafi zinazopatikana nchini kama mchanga, chokaa, felsper na magadi soda kutoka nje ya nchi kwa sasa.

Pia, amesema 40% ya chupa hizo hutengwnezwa na mabaki ya chupa zilizotumika hivyo amewaomba wanachi kukusanya kwa wingi mabaki ya chupa zilizotumika ili kurahisisha upatikanaji wa malighafi ya uzalishaji wa chupa hizo na kutunza mazingira.

Naye, Meneja wa Utawala Bwana Kapil Dave amesema kampuni hiyo iko tayali kuunga mkono juhudi zozote zinazofanywa na Serikali ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner