Ad imageAd image

DKT. Mwinyi awahakikishia Wawekezaji wa EU mazingira rafiki ya Uwekezaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ametoa wito kwa Wawekezaji wa Umoja wa Ulaya kuja kuwekeza nchini na kuwahakikishia mazingira ya Uwekezaji ni mazuri na yanazidi kuboreshwa.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akifunga Jukwaa la Uwekezaji na Biashara baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Aidha Dkt. Mwinyi amesema Umoja wa Ulaya ni moja ya Wawekezaji wa Mstari wa mbele nchini Tanzania na kuongeza kuwa anaamini kuwa Jukwaa la biashara baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ni chachu ya kukuza ushirikiano kati ya Umoja huo na Tanzania.

Zaidi ya watu 800 kutoka nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya na Makampuni zaidi ya 150 kutoka Tanzania wamehudhuria katika Mkutano huo.

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner