Baada ya kadi kutengenezwa, kadi pepe iko tayari kutumika kwa malipo ya mtandaoni.” Alisema Pesha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji alifurahishwa na ushirikiano huo muhimu.
“Selcom, tunajivunia dhamira yetu isiyoyumba ya uvumbuzi na ubora katika sekta ya malipo. Tunayofuraha kuungana na washirika kama Tigo Pesa na Mastercard kuzindua huduma hii iliyounganishwa na Akaunti ya TigoPesa. Kwa kuwekeza mara kwa mara katika miundombinu yetu na kuboresha uwepo wetu wa soko. Tunalenga kutoa masuluhisho ya kisasa, yanayotegemewa ambayo yanakuza ukuaji na mafanikio kwa washirika wetu na wateja vile vile.”
Naye Ngozi Megwa, Makamu wa Rais Mwandamizi, Ushirikiano wa Kidijitali EEMEA, Mastercard alisema,
“Mastercard inatambua kuwa watumiaji leo wanatafuta bidhaa rahisi na salama za kifedha ambazo zinaongeza thamani zaidi katika maisha yao ya kila siku. Mbinu yetu ya ubunifu inalenga kuwezesha mageuzi ya kidijitali ya washirika wetu ili mamilioni ya wateja waweze kufurahia ufikiaji wa mfumo wa malipo wa kimataifa wa malipo na uzoefu bora wa mtumiaji. Teknolojia yetu imetayarishwa kikamilifu ili kuwawezesha washirika wetu kuzindua masuluhisho ya kibunifu na yanayofaa ambayo yataunda pendekezo dhabiti la thamani kwa wateja wetu wote. Pamoja na uhusiano wetu ulioimarika na wahusika wa sekta ya mawasiliano ya simu, ushirikiano huu na Tigo unajumuisha dhamira yetu ya kupanua zaidi chaguo la wateja na ufikiaji wa biashara ya kidijitali.”
Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kuomba kadi pepe kutoka kwenye menyu ya Tigo Pesa kwa kupiga *150*01#, kisha uchague Huduma za Kifedha (7), Chagua Kadi za Tigo Pesa (7), Chagua Tigo Pesa MasterCard (1) ili kuendelea. APP ya Tigo Pesa Chagua Huduma za Kifedha, Chagua Kadi za Tigo Pesa, kisha Chagua Tigo Pesa MasterCard ili kuendelea.
Zaidi ya hayo; Tigo Pesa itawapa wateja wake chaguo nyingi za kutengeneza kadi, ambazo ni; Kadi ya Matumizi ya Mara Moja na Uhalali ambayo ina chaguo la Siku 90. Baada ya kadi kuundwa, kadi pepe iko tayari kutumika kwa malipo ya mtandaoni.

