Ad imageAd image

TUMIENI MAARIFA YA USHIRIKA KUJIJENGA KIUCHUMI – Profesa. Nkonoki

Mkurugenzi wa Kituo cha Kanda ya Ziwa - Mwanza
Highlights
  • "Ndugu washiriki ninawaomba mkatumie mbinu za uongozi mlizozipata kuviwezesha vikundi na vyama vyenu vya ushirika kupata uchumi imara kwa mstakabali wa ushirika na mtu mmoja mmoja". Alisema Prof. Nkonoki.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa akimkabidhi Mshiriki wa Mafunzo Cheti cha Ushiriki
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa akimkabidhi Mshiriki wa Mafunzo Cheti cha Ushiriki

Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzi cha Kanda ya Ziwa Mwanza, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Juvenal B. Nkonoki amevihimiza vikundi vya Wavuvi na Wachakataji Dagaa vya Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kutumia maarifa ya ushirika waliyo yapata kujijenga KIUCHUMI.

Wito huo umetolewa Ijumaa Septemba 22, 2023 katika hafla ya ufungaji wa mafunzo yaliyo fanyika kwa siku mbili ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa vyama vya ushirika na vikundi 10 vya Wavuvi na Wachakata Dagaa vyenye jumla ya Wanachama 1058 kati yao Wanawake 185 na Wanaume 873. Mafunzo hayo ya misingi ya ushirika kwa vyama vya ushirika na vikundi yamefanyika katika Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani.

“Ndugu washiriki ninawaomba mkatumie mbinu za uongozi mlizozipata kuviwezesha vikundi na vyama vyenu vya ushirika kupata uchumi imara kwa mstakabali wa ushirika na mtu mmoja mmoja”. Alisema Prof. Nkonoki.

Profesa Nkonoki ameendelea kuishukuru Serikali ya Japani pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ufadhili wa mafunzo hayo pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa uratibu wa mafunzo hayo yaliyo fanyika katika Wilaya za Mafia, Pangani na Bagamoyo.

Wakati huo huo mwakilishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Owen Kibona.amevitaka vikundi hivyo kutunza na kuzilinda rasilimali za uvuvi kwa kutumia njia sahihi ambayo Wizara inapendekeza.

Nae Mrajisi Msaidi wa Mkoa wa Pwani Bw. Abdilah Abasi amewapongea Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Chuo cha Mipango kwa uratibu wa mafunzo hayo elekezi kwa vikundi na vyama vya ushirika vya wavuvi vya Mkoa wa Pwani.

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo Wavuvi na Wachakataji wa Dagaa ni moja kati ya Malengo ya mradi wa kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu Nchini unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Chuo cha Mipango.

Share this Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

adbanner